• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Mahesabu
      • Maendeleo ya Jamii na Huduma ya Lishe
    • Vitengo
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Mahesabu
    • Kata
      • BAGA
      • BUMBULI
      • DULE B
      • KISIWANI
      • KWEMKOMOLE
      • MAHEZANGULU
      • MAMBA
      • MAYO
      • MGWASHI
      • MILINGANO
      • MPONDE
      • NKONGOI
      • SONI
      • TAMOTA
      • USAMBARA
      • VUGA
      • KWEMAKONKO
      • MBUZII
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Utalii
    • Viwanda
    • Biashara
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma
    • Ushauri katika Kilimo
    • Ushauri katika Mifugo
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Ujasiriamali na Utoaji Mikopo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyopangwa
    • Miradi Inayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Vitega Uchumi vya Halmashauri
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Fomu
    • Makala
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

Miundombinu, Maendeleo Mjini na Vijijini

Idara hii ina majukumu ya kusimamia na kushauri masuala yote yanayohusu miundombinu katika Halmashauri. Malengo tajwa yatafikiwa kwa Idara kutekeleza kazi zifuatazo: -

  1. Kushauri kuhusu masuala ya sekta ya ujenzi;
  2. Kupanga maendeleo ya miundombinu;
  3. Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo ya wakandarasi;
  4. Kukagua kazi za ujenzi zinazofanywa na Halmashauri na kuhakikisha ubora wake;
  5. Kutoa vyeti kwa wakandarasi kwa mikataba iliyokamilika;
  6. Kufanya uwekaji lami wa barabara mpya kwa kushirikiana na TARURA;
  7. Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na Taasisi za nje na ndani ya nchi zinazoshughulikia masuala ya miundombinu;
  8. Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi;
  9. Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi; na
  10. Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya Ardhi.


Idara hii inaundwa na Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo: -

  1. Sehemu ya Ujenzi;
  2. Sehemu ya Barabara; na
  3. Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini.


Sehemu ya Ujenzi:

Sehemu hii inatekeleza shughuli zifuatazo: -

  1. Kutoa ushauri wa sheria, kanuni, taratibu na mambo yote yanayohusu ujenzi;
  2. Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za masuala ya ujenzi;
  3. Kuandaa mikataba inayohusiana na majengo na mitambo;
  4. Kutayarisha na kukadiria gharama za ujenzi;
  5. Kufuatilia utendaji kazi wa wakandarasi;
  6. Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
  7. Kukagua majengo na kuhakikisha ubora wake;
  8. Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba; na
  9. Kusimamia uendeshaji wa warsha za Halmashauri.


Sehemu ya Barabara:

Sehemu hii inatekeleza shughuli zifuatazo: -

  1. Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na utambuzi na uwekaji lami wa barabara mpya;
  2. Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni kwenye barabara za lami;
  3. Kutengeneza barabara mpya katika ardhi iliyopimwa;
  4. Kuandaa mikataba ya uwekaji lami wa barabara mpya;
  5. Kutayarisha makadirio ya gharama za kuweka lami barabara;
  6. Kufuatilia utendaji wa wakandarasi;
  7. Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba;
  8. Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
  9. Kukagua barabara za lami ili kuhakikisha ubora; na
  10. Kusimamia ujenzi na matengenezo ya vituo vya mabasi.


Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini:

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-

  1. Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
  2. Kusimamia huduma za kimazingira na kijamii;
  3. Kuongoza mipango ya maendeleo ya miji, makazi na matumizi endelevu ya ardhi;
  4. Kusimamia na kuratibu usimamizi wa mambo ya kale na utalii;
  5. Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
  6. Kuratibu na kukuza maendeleo ya miji inayochipukia kutoka vijiji hadi makazi ya mijini; na
  7. Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi.

Matangazo

  • No records found
  • View All

Habari Mpya

  • Wasiliana na jukwaa la Vijana

    January 28, 2026
  • NMB makao makuu wakutana na timu ya Bumbuli

    October 25, 2025
  • UFUNGUZI WA UGAWAJI WA MIKOPO YA 10%

    September 01, 2025
  • MAFUNZO KWA WATAALAMA WA MIFUGO

    May 30, 2025
  • View All

Picha Jongefu

MFUMO WA MIKOPO YA 10% - NAMNA YA KUJISAJILI
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • FURSA ZA KILIMO CHA CHAI
  • USHAURI KATIKA MASUALA YA KILIMO
  • FURSA KATIKA MASUALA YA MIFUGO
  • FOMU YA MAOMBI MBALIMBALI
  • ELIMU YA UJASIRIAMALI NA UTOAJI WA MIKOPO
  • ORODHA YA WAHESHIMIWA MADIWANI
  • RATIBA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI

Viunganishi Linganifu

  • TOVUTI KUU YA IKULU
  • TOVUTI YA OR-TAMISEMI
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli

Wasiliana Nasi

    02 KITONGOJI CHA UGUNGA

    Postal Address: S.L.P 111, BUMBULI

    Telephone: 0272977530

    Mobile:

    Email: ded@bumbuklidc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.